Binti mmoja anaeitwa Latifa inasemekana alivamiwa na majambazi na kuuwawa katika kijiji cha Tamau Ziwani na hatmae kuzikwa mwishoni mwa january 2024.
Hata hivyo taarifa za kifo hicho zilipelekwa kijijini kwao Nyamigunga Bunda na hivyo familia akiwemo mama yake bi Tatu Muhoja Nkondo ilifanya taratibu zote husika katika vyombo husika na kwenda katika kijiji cha Tamau kufukua maiti hio na kwenda kuizika kijijini kwao Nyamigunga
Hata hivyo chombo hiki cha habari kiliongea na mwenyekiti wa ukoo huo mitandaoni bw James Nyanda ametuthibitishia kuwa baada ya wiki moja ya mazishi bi Latifa alizua taharuki baada ya kurudi akiwa mzima
Hivi sasa familia imetoa ripoti sehemu husika kuomba kama kuna familia imepoteza mja wake waende wakafukue maiti hio kwani sio ya Latifa itakuwa kazikwa mtu mwingine



0 Comments