Blog Post

KAUSHA DAMU NYINGINE ZIMEZUKA MITANDAONI



 

Hivi karibuni Wizara ya Fedha ilionya taasisi binafsi na makampuni na watu binafsi  wanaokopesha wananchi kwa riba kubwa, bila kufuata taratibu za kisheria na kusajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT),  na kuwataka wafate sheria

Aliekuwa naibu waziri wa fedha Mhe Ashantu Kijaji alisema"Tunakwenda kutumia sheria ndogo za huduma ya fedha kuwanusuru watanzania kwani wakopeshaji hao wanatumia riba ya juu kandamizi ."

Gazeti la Chama cha Mapinduzi CCM la hivi karibuni liliandika taarifa hiyo, lakini bado kumekuwa na makampuni na watu binafsi wengi wanaibuka kukopesha watu kwa riba kubwa na kuendelea na mikopo ya kausha damu nchini.

Blog hii inaendelea kufuatilia makapuni hayo na kuendelea kufichua mambo yanafanywa kinyume na sheria.
Baadhi ya wananchi wanasema hawa Wakopeshaji mitandaoni wanatumia umasikini wa mtu na hivyo kumnyanyasa kimasilahi 

Inasemekana mikopo hio ina riba zaidi ya nusu ya pesa iliokopwa kwani mwananchi mmoja  leo hii alikopeshwa shilingi elfu hamsini na nane na kuambiwa alipe shilingi elfu tisini na kwa muda wa wiki moja tu jambo ambalo riba hio ni zaidi ya nusu ya pesa aliekopa. Blog hio inao ushahidi huo 

Bwana mmoja amesema hata masharti wanayotoa yanatia mashaka yanaweza kutumika vibaya kama vile wakopeshaji hao kupata uwezo wa kufuatilia meseji zote na simu za watu wengine ambao hawahusiki na mkopo huo

Hata hivyo Blog hii inaendelea na uchunguzi pia kuzungumza na BOT na TCRA na mwisho wa uchunguzi tutaweka bayana majina ya kampuni hizo na nini hasa malengo yao .
kunukuu

Post a Comment

0 Comments

Close Menu