Blog Post

SERA YA MAMBO YA NJE KUBORESHWA


 


Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki 

Na Omar Mbarak

Kongamano kubwa la maboresho ya sera ya mambo ya nje linatarajia kufanyika mwezi huu kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoa maoni yao.

Kwa mujibu wa mwaliko wa kushiriki kongamono hilo uliotolewa kwa wadau mbalimbali na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kongamano hilo litahusu Maboresho ya Sera mpya ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001

Kongamano hilo litashirikisha wadau mbalimbali kutoa maoni kuhusu maboresho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 na Mkakati wake wa Utekelezaji.

Kwa mujibu wa wizara hiyo kongamano hilo litakalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 9 Januari, 2024 kuanzia saa 3.00 asubuhi.*

“Lengo la Kongamano hilo ni kupata maoni ya wadau katika maeneo mapya yanayopendekezwa katika Sera ya Mambo ya Nje inayofanyiwa maboresho na pia maeneo mengine yaliyopo ambayo yanaendelea kutekelezwa kama yalivyokuwa katika Sera ya Sasa.” Inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Wizara hiyo imetoa wito kwa wadau na kuwaalika wadau wote ikiwa ni pamoja na; Wanachuo/Wasomi, Wanasiasa, Vyama vya Siasa, Taasisi za Kidini, Asasi za Kiraia, Taasisi Zisizo za Kiserikali (NGOs) na wananchi kwa ujumla kushiriki Kongamano hilo muhimu litakalosaidia kukusanya maoni yatakayowezesha kupata Sera imara ya Mambo ya Nje.* 

 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu