Blog Post

Mashaka Matongo 'Abiola' afariki dunia



Na Mdoe Kiligo

ALIYEKUWA Mchapishaji na Mkurugenzi wa magazeti mbalimbali Mashaka Matongo "Abiola" amefariki Dunia leo Desemba 19, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za ndugu wa karibu wa marehemu zinasema kwamba Mashaka amefariki Dunia leo na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho Yombo Dovya, Wilayani Temeke.

Abiola alikuwa maarufu tangu alipokuwa wakala wa magazeti na vitabu na baadaye akapanda chati zaidi baada ya kuanza kuchapisha na kumiliki magazeti kadhaa,.

Baadaye' akawa Rais wa Wasanii huku pia akishiriki kucheza baadhi ya filamu akishirikiana na Wasanii mbalimbali.




Post a Comment

0 Comments

Close Menu