Na Omar
Mbaraka
Hivi
karibuni Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),
alisema kuwa asilimia sabini ya wagonjwa waliolazwa wodi za taasisi hiyo
wanatokana na ajali za pikipiki maarufu kama bodaboda.
Hivyo basi
kutokana na taarifa hiyo ya kushtua
ilipelekea kwenda kuwatembelea majeruhi wa ajali katika hosptali ya MOI, lengo
kubwa lilikuwa ni kuwapa pole na kujua kulikoni!
YALIOJITOKEZA
Kati ya wagonjwa
wa majeruhi wa ajali za bodaboda niliobahatika kuwatembelea katika taasisi ya MOI baadhi walikuwa ni abiria na wengine
walikuwa ni madereva wa bodaboda.
Baadhi ya
majeruhi tayari wamekuwa wamepata ulemavu wa kudumu hata baada ya kuruhusiwa
kutoka hosptali atakuwa akitembelea magongo au baskeli ya walemavu
(wheelchair), jambo ambalo hatoweza
kufanya kazi tena zaidi ya kuwa tegemezi kwa familia na Taifa kukosa nguvu kazi
Baada ya
kufanya utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa ukiukwaji wa sheria kama vile
kupakia abiria zaidi ya mmoja, maarufu kama mshikaki na kukimbia mwendo kasi,
pikipiki inapakia watu wanne jambo ambalo linasababisha dereva wa bodaboda
kukosa balance na hivyo kusababisha ajali. Pia huku wakikiuka sheria za barabarani kwa kupita wakati wa taa nyekundu
Kutokana na
kukiuka sheria za barabarani madereva wa bodaboda wamekuwa wakisababisha
seriakali badala ya kupoteza nguvu kazi ya mtu mmoja iwapo atapakia abiria
mmoja akipata ajali, sasa badala yake inapoteza nguvu kazi ya watu wanne kwa kupakia
mshikaki.
Utafiti
unaonesha kuwa kuna baadhi ya bodaboda hufunga honi za magari makubwa, jambo
ambalo limekuwa kero kwa wananchi na linaweza kuwa sababu ya magonjwa ya
shinikizo la moyo kuongezeka na kusababisha presha na mshutuko kwa watu kwani honi hizo
zimekuwa zikipigwa bila mpangilio barabarani.
Honi hizo za
magari makubwa zinazofungwa na dereva wa bodaboda zimekuwa kero kubwa sana
baadhi ya dereva wa bodaboda wakifika karibu na magari hupiga honi hizo na
kushtua dereva wa gari akidhani kuwa kuna gari kubwa linakuja nyuma yake na hivyo kujaribu kulikwepa na matokeo yake kusababisha ajari.
Madereva wa bodaboda wanaofunga honi hizi wanakiuka kanuni kwa sababu wataalam
waliotengeneza bodaboda hizi hawakufunga honi za magari makubwa kutokana na
matumizi ya vyombo hivyo havistali kuwa na honi kubwa zenye kushtua watu.
USHAURI
Neno la
bodaboda limetokana na nchi ya jirani ya Uganda lina maana ya ‘boarder to
boarder’ likiwa na maana ya mpaka hadi mpaka, hivyo basi tafiti zinaonesha kuwa baadhi ya
nchi jirani kama vile Uganda na Rwanda madereva wa bodaboda wanapewa mafunzo ya
usalama barabarani na wanaongoza kwa kutii sheria za barabarani na hivyo ajali katika nchi hizo zimepungua
sana.
Pamoja na
ukweli kuwa usafiri wa bodaboda ni muhimu na unasaidia kupunguza tatizo la
ajira hapa nchini, hivyo viongozi wanatakiwa kuhimiza bodaboda kuchukua mafunzo
ya usalama barabarani, kutii sheria za barabarani, pia plate namba za bodaboda ziwe
na rangi maalum ili askari wa usalama barabarani iwe rahisi kudhibiti bodaboda za kupakia abiria. Hivyo badala ya viongozi kuhimiza
ajira za bodaboda badala yake pia wahimize madereva wa bodaboda kupewa mafunzo kwanza ya sheria za barabarani
Kuedelea
kuhimiza bodaboda kama njia ya kuongeza ajira kwa vijana bila kutoa mafunzo ya usalama barabarani na kutii sheria inapelekea kusababisha kuongezeka kwa umaskini katika
familia kutokana na familia nyingi kuwaghalamikia majeruhi mamilioni ya shilingi na kupoteza nguvu kazi ya Taifa kwa ajali za bodaboda
ambazo zinazidi kuongezeka kila kukicha
0 Comments