Na Omar
Mbarak
Wakala wa
Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), inazidai
taasisi mbalimbali za serikali zaidi ya shilingi bilioni 39 na hivyo kushindwa
kuzilipa kampuni binafsi za wazawa zilitoa huduma kwenye taasisi mbalimbali za serikali.
Kutokana na
uchunguzi uliofanywa na blog hii unaonesha makampuni mbalimbali ya binafsi
yalitoa huduma mbalimbali zikiwemo za kusambaza vifaa mbalimbali zikiwemo
nyanya za umeme, zinaidai TEMESA zaidi ya bilioni 39.
Kutokana na
taasisi mbalimbai za serikai kushindwa kuilipa TEMESA kwa wakati, TEMESA
inashindwa kuwalipa wazabuni hao kwa wakati na hivyo kusababisha malalamiko kwa
wazabuni na chuki kwa serikali yao.
Mwandishi wa habari hizi alipoongea na baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakifuatilia madeni yao Makao Makuu ya TEMESA jijini Dodoma, baadhi wanasema kuwa wana hofu ya kufilisiwa na benki ambazo walikopa mikopo baada ya kushindwa kurejesha mikopo yao kwa wakati kutokana na malipo yao kuchelewa kwa muda mrefu baada ya kutoa huduma kwenye taasisi za serikali.
Wanasema
kutokana na kushindwa kulipwa malipo yako kwa wakati baadhi yao watoto wao
wamekatisha masomo kwa kujiunga na vyuo hivyo hatua ambayo inapelekea kuanza kujenga
chuki na serikali yao lakini hawana la kufanya.
Mfanyabishara
mmoja ambaye ni Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM ambaye hakupenda kutaja jina lake, anasema kuwa serikali ni mali
ya CCM na watendaji wa taasisi za
serikali wanaosababisha uzembe huu wa kuchelewesha malipo yao yanaweza kupelekea
kura kwa CCM wakati wa uchaguzi ujao kupungua.
“Deni la
bilioni 39 ni kubwa na linajumuisha na kuhusisha familia nyingi,” anasema Kada
huyo wa CCM.
Hivyo
amezitaka taasisi hizi za serikali ambazo zilipewa huduma na makampuni binafsi
kulipa mapema TEMESA ili iweze kuwalipa wadai wake.
Majukumu ya msingi ya TEMESA ni kufanya matengenezo ya Magari, pikipiki na Mitambo ya Serikali katika Karakana ambazo zipo kila Mkoa
Kufanya
matengenezo na Usimikaji wa Mifumo ya Umeme, Mabarafu, viyoyozi na Elektroniki,
Kufanya matengenezo ya taa za kuongozea magari (Traffic Signals) na taa za
barabarani (Street Lights)
Kukodisha magari kwa ajili ya usafiri wa Viongozi (VIP Vehicles) yaliyopo katika Kitengo cha GTA (Government Transport Agency) ;
Kukodisha mitambo ya kuzalisha kokoto, na mitambo ya kazi za
barabara;
Uendeshaji wa Vivuko vya Serikali; Kutoa ushauri wa Kitaalamu kwa Serikali na Umma kwa ujumla katika nyanja za uhandisi wa Ufundi, Umeme na Elektroniki; utoa ushauri wa kitaalamu kuhusu usimikaji wa mifumo mipya ya uhandisi wa Ufundi, Umeme na Elektroniki; na
Kufanya usanifu na Usimamizi wa usimikaji wa mifumo ya uhandisi
wa Ufundi Umeme na Elektroniki ili kukidhi viwango vinavyotakiwa na kwa
kulingana na matakwa ya Sheria na Taratibu zinazoongoza taaluma husika.
0 Comments