Blog Post

CHONGOLO AJIUZULU CCM



Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Daniel Chongolo

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, amejiuzulu nafasi yake hiyo baada ya kukitumikia chama hicho kwa takribani miaka miwili na nusu.

Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho jioni ya leo inaeleza Chongolo aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa chama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Katika kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam, Rais Samia amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwake, na ameridhia ombi hilo.

Chongolo aliteuliwa katika nafasi hiyo mwezi April 2021akimrithi Dkt. Bashiru Ally. Chongolo ni miongoni mwa Makatibu Wakuu wa CCM waliohudumu kwa muda mfupi.

Katibu Mkuu aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi ni Wilson Mukama ambaye alidumu kwenye nafasi hiyo kwa mwaka mmoja na miezi saba, kati ya Aprili mwaka 2011 na Novemba mwaka 2012

Post a Comment

0 Comments

Close Menu