Katika mahafali hayo ambayo yalifana sana mkuu wa chuo Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe Abeid Amani Karume ndie alietunuku shahada hizo kwa madaktari wa fani mbalimbali wakiwemo madaktari bingwa.
Mmoja wa wahitimu aliewakilisha wahitimu wa shahada za awali bw Whitefrank M Frank katika hotuba yake alisema nanukuu "Kwa wazazi na walezi wetu, leo tumetimiza ahadi ya uaminifu kwenu na fani hizi zikawe zawadi kwenu kwa kujitoa kwenu kuhakikisha tunapata urithi bora wa elimu.Zaidi ya yote tunarudisha sifa na shukurani kwa mwenyezi mungu kwa kutupa nafasi ya kufanya haya.
Hivyo basi jana ilikuwa pia ni furaha kwa wazazi wa madaktari hao kama uonavyo katika picha hapa chini Mzee Omar Mbaraka na bi Zuhura Abdi wakiwapongeza watoto wao Dr Abdallah Bakari Shekhalage kuwa daktari bingwa pua, koo na masikio(Otorhinolaryngologist/ENT Surgeon) na Dr Warda Omary Mbarak kupata masters of Radiology (Radiologist)
0 Comments