Blog Post

BARABARA YA MOROGORO YAJAA MAJI YA MVUA


Hapa ni Dar es Salaam, Tanzania. Hii ni Morogoro Road, ni barabara iliyoanzishwa na wakoloni wa Kiingereza mwaka 1932 baada ya kutunga sheria ya High Way Ordinance cap 167

 Barabara ya Morogoro ina urefu wa kilometa 1,300 ikianza katika ofisi za Jiji la Dar es Salaam karibu na bahari ya Hindi hadi Tunduma, Songwe mpakani na Zambia.

 Kwa mujibu wa sheria ya High Way Ordinance cap 167 tofauti na barabara nyingine, barabara hii imekuwa na hifadhi yenye upana tofauti kuanzia mita 22, 180, 243. Ukitoka Dar es Salaam zilipo ofisi za Jiji ina upana wa mita22, lakini ukifika Ubungo hadi Kimara ina upana wa mita 90 kila upande kutoka katikati ya barabara. Mita 180. Kutoka Kimara Stopover hadi TAMCO-Kibaha, upana ni mita 121.5 kila upande kuanzia katikati ya barabara.

Hivyo ukubwa wa hifadhi kuongezeka kufika mita243. Unaweza kuona, hii barabara ni muhimu sana kuanzia katikati ya Jiji la Dar es Saalam hadi kufika nje katika mkoa wa Pwani hadi Tunduma-Songwe. Barabara ya kimkakati. 

 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu