Blog Post

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AKABIDHI MTUMBWI


Na OMAR MBARAK

Naibu Waziri wa Fedha na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, NEC, Hamad Hassan Chande, amekabidhi msaada wa mtumbwi kwa kikundi cha Fasta Fasta Pemba visiwani Zanzibar.

Mhe. Chande ambaye ni mbuge wa jimbo la Kojani, alitoa msaada huo kwa kikundi hicho mtumbwi unafahamika kwa jina la Faiba wenye uwezo mkubwa ikiwa na taaluma nane yenye mashine ya hozi pawa 15 yenye uwezo wa kufika sehemu yoyote kwenye bahari.

Akizungumza wakati wa kukabidhi boti hiyo kiongozi wa kikundi cha Fasta Fasta Musa Omar Mgawu alishukuru msaada huo na kuahidi kutekeleza ahadi zao kwa Mhe. waziri kuendelea kuunga mkono serikai na chama hicho kwa kumpa kura zote.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu