Tarehe 27 April 2023 lilitokea tukio la kusikitisha baada ya wafanyakazi wawili kumwagikiwa na uji wa chuma wa moto wa kutengenezea nondo katika kiwanda cha Hang Jin Company Limited kinachomilikiwa na raia wa China kilichopo Kisemvule wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.
Tafakari news weblog hivi karibuni ilipata nakala ya barua ilioandikwa na mmoja wa wafanyakazi kwenda kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dr Samia Suluhu Hassan ambayo mbali na kuelezea tukio hilo ilielezea kuminywa kwa haki nyingi za wafanyakazi katika kiwanda hicho yakiwemo kutopewa vitendea kazi, kutopewa mikataba ya ajira,kufanyishwa kazi masaa ya ziada bila kulipwa (Overtime)
Hata hivyo katika kutafuta ukweli Tafakari news ilianza kwanza kwenda kwa mkuu wilaya karibu kwa siku mbili bila kuonana nae hatimae tulifanikiwa kuzungumza na kaimu afisa utawala ambae pia ni Afisa tarafa wa eneo lilipotokea tukio la Kisemvule bw Muya Hata hivyo nae alisema hajasikia tukio hilo ila alitupatia baraka kwenda kuonana na uongozi wa kiwanda hicho
Baada ya kufika kiwandani hapo tulipokelewa na kuongea na afisa muajiri(HR) bw Anjetile Henzron Mwakusya ambae alikili kutokea kwa tukio hilo tarehe 27 April 2023 kwa wafanyakazi wawili ambao walikimbizwa hospitali na tarehe 28 April 2023 mmoja wapo bw Abdallah Kunja tarehe 28 April 2023 alifariki dunia katika hospitali ya rufaa Muhimbili na mwingine bw Juma Lwambo ametibiwa na kupona
Kuhusu haki zao za msingi Mwakyusa alisema familia ya marehemu Kunja yenye watu 24 walidai walipwe fidia ya t shs milioni thelathini ambazo wamelipwa na kusaini wote
Hata hivyo Tafakari news ilizungumza na mdau mmoja ambae alisema matukio kama haya yanatokea mara kwa mara hapa wilayani mkuranga na kutoa mfano raia mmoja wa china kumsakizia mfanyakazi mmoja ambae alijeruhiwa vibaya na mbwa.Anadai yote haya ni kwa vile hawatembelewi viwandani na maafisa wa kazi toka serikalini na kuwaelekeza taratibu za kazi. Alisema Afisa kazi yupo mbali kibaha ambae hupita mara moja kwa miezi mitatu.
0 Comments