Nchi yetu ina rasilimali nyingi sana yakiwemo madini aina mbalimbali kama vile dhahabu, almasi, lubi, makaa ya mawe,Tanzanite (ambayo hakuna duniani isipokuwa Tanzania), gas, petrol nk
Kuna nchi kama vile za kiarabu zimekuwa na rasilimali ya mafuta (petrol, diesel nk) katika ardhi yao, lakini zamani nchi hizo zilikuwa masikini na wasomi wachache sana
Hata hivyo walichofanya ni kuwakaribisha nchi za ulaya kama vile marekani na uingereza nk kuja kuchimba mafuta hayo kwa makubaliano ya kugawana kipato matokeo yake nchi hizo sasa hivi zimekuwa tajiri kupindukia baadhi zimekuwa zikiwalipa mishahara raia wake bila kufanya kazi na baadhi kama vile Libya mtu akioa anajengewa nyumba
Hivyo basi hapa Tanzania tunahitaji kiongozi wa nchi atakae kuwa mbunifu kuinua uchumi wetu kupitia rasilimli zetu kama vile bandari, mbuga za wanyama,madini nk
Hivyo basi wananchi wa Tanzania hatuna budi kumsifu Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa ubunifu wa kuongeza mapato yetu kupitia bandari yetu anastahili pongezi badala ya kumtupia lawama
Inasemekana bandari yetu hivi sasa inaingiza t shs trilioni saba lakini baada ya ubia na DP world itaingiza t shs trilioni ishirini na saba na kuweza kuchangia asilimia sitini na saba ya bajeti yetu kwa mwaka hakika huu ni ubunifu mkubwa
Hata hivyo baada tu ya huu ubunifu mkubwa kuna baadhi yetu kwa utashi wao kisiasa wengine kimasilahi wamekuwa wakimwaga sumu ili ubunifu huu usiendelee
Kwa upande wa kimasilahi inasemekana hapo awali mtu akiajiriwa hata kwa cheo kidogo mlinzi au katibu mukhtasi kwa muda mfupi tu anaweza kumiliki nyumba mbili au zaidi na wale wa vyeo vya juu wanakuwa mamilionea,hivyo basi si ajabu watu kama hawa kumwaga sumu kuhisi kuwa ndio mwisho wa maisha yao ya kifahari
Kwa upande wa siasa ni nafasi yao nzuri kueneza agenda yao mbaya ili kuupakazia ubunifu huu mzuri ili wapande kisiasa bila kujari masilahi ya nchi
Ubunifu mwingine wa mama Samia ni ule wa filamu ya Royal tour ambao tayari umetuingizia kipato kikubwa kutokana na watalii wengi kuja hapa nchini. Hakika sasa tunae Rais mbunifu Dr Samia Suluhu Hassan
Ni uchambuzi wa Omar S Mbarak
0 Comments