Blog Post

CCM kuendelea kushirikiana na waandishi kuleta maendeleo


 Na Mwandishi Wetu

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Edward Mjema  amekutana na kuzungumza na vyombo vya habari mbalimbali vya  habari hapa nchini.

Mjema amekutana na waandishi wa habari wa Magazeti, Televisheni, Redio na Blogu) nchini katika kuhakikisha  mahusiano baina ya CCM na wanahabari yanazidi kuwa bora na kuendelea kuimarika, kulingana na mahitaji ya wakati.

Chama Cha Mpainduzi kitaendelea kutambua umuhimu na nafasi ya vyombo vya habari  katika kueneza Sera na Itikadi ya Chama cha Mapinduzi na kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM na utendaji kazi wa Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu