Blog Post

Ridhiwani awakaribisha wakorea Chalinze



Na Mwandishi Wetu


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amekutana na viongozi wa Taasisi ya Wakolea inayoitwa Kofih Tanzania.

Ridhiwan ambaye ni mbunge wa jimbo la Chalinze, amefanya mazungumzo na viongozi wa taasisi hiyo hapa nchini Tanzania hivi karibuni kufanikiwa kuwashawishi kuboresha huduma za afya.


Akizungumzia mkutano huo Ridhiwani alisema mkutano huo ulilenga masuala mbalimbali ya kuboresha maendeleo hususani huduma za afya hapa nchini.

"Tumekuwa na mkutano mzuri na Taasisi ya Wakorea inayoitwa Kofih Tanzania. Tumekubaliana ushirikiano kwa miaka mitano", alisema.

Mkutano huo ulilenga kuimarishwa kwa miundombinu ya Afya hasa hosptali ya wilaya, vituo vya afya na kuwezesha vifaa tiba katika eneo la kina mama na watoto.

Ridhiwani ambaye tangu kushika nafasi ya ubunge wa jimbo la Chalinze amekuwa akilenga zaidi katika maendeleo ya jimbo hilo katika upande wa afya na miundo mbinu.

Akizungumzia mkutano huo wa taasi ya Wakorea alisema umelenga kuboresh huduma na mahitaji ya vifaa vya huduma za dharura na kuwezesha watendaji wa sekta mafunzo ya ujuzi wa juu katika halmashauri ya Chalinze.

0753737777


 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu