Blog Post

WAZIRI MHE KAPINGA ASEMA VIWANDA VYA PUNGUZA UTEGEMEZI WA BAADHI YA BIDHAA ZA NJE KWA TRILLIONI 6.2

 Na Mwandishi wetu 

Dodoma 


Serikali imeeleza kuwa utekelezaji wa Sera ya Viwanda ya mwaka 1996 umezalisha mafanikio makubwa kupitia Viwanda vya kimkakati vilivyopunguza takribani Shilingi trilioni 6.2 kwa mwaka kwa bidhaa nne pekee za Saruji,Nondo,Vigae na Mabati kama vingenunuliwa kutoka nje ya nchi.


Akizungumza tarehe 4 Novemba 2026,Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Sera ya Maendeleo endelevu ya Viwanda ya Mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Jasiriamali wadogo na za wa kati ya mwaka 2003 (Toleo la Mwaka 2025),Waziri wa Viwanda na Biashara,  Mhe.Judith Kapinga, amesema uzalishaji wa ndani wa bidhaa hizo umezidi mahitaji ya nchi na kuweka msingi imara wa kujitegemea kiuchumi,aidha,amebainisha kuwa mafanikio hayo yanatoa mwelekeo mzuri katika kuanza kwa utekelezaji wa sera mpya zinazolenga kuendeleza Maendeleo endelevu ya Viwanda na Wajasiliamali nchini.




Post a Comment

0 Comments

Close Menu