Blog Post

MKUU WA WILAYA YA MUFINDI ASTAHILI PONGEZI

 Na Omary Mbaraka 

MAKALA  MAALUM 

MKUU WA WILAYA YA MUFINDI NA TIMU YAKE WASTAHILI PONGEZI

Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Lina Selekwa na kikosi Cha ulinzi wilayani hapo walifanikiwa kukamata kiwanda bubu kinachotengeneza pombe Kali feki zikiwemo aina ya Konyagi na  nyinginezo eneo la pipeline Mafinga

Kitendo alichofanya mkuu huyu wa wilaya pamoja na timu yake sio TU Cha kizalendo pia wameokoa maisha ya binadamu wengi kwani mchanganyiko WA pombe hii Kali feki ni rahisi kusababisha maradhi ya aina nyingi kwa binadamu  ikiwemo maradhi ya kansa ambayo yameua watu wengi hapa nchini na duniani

 Pia kitendo hiki  kimeokoa mianya ya kupotea kwa fedha za serikali zikiwa ni Kodi kwani pombe hio feki ilikuwa Ina changia kushuka kwa mauzo ya viwanda halali ambavyo vinalipa Kodi serikalini na mengineo mengi

Hivyo chombo hiki Cha habari kinatoa pongezi nyingi kwa mkuu WA wilaya ya mufindi na timu yake nzima ya ulinzi "Kazi iendelee"

Na kwa utafiti uliopo pombe Kali hizi feki zinatengenezwa na kuuzwa katika mikoa mingi hapa nchini, na vinavyozidi kuwepo mbali na serikali kupoteza Pato lake pia serikali inazidi kupoteza nguvu KAZI yake tokana na maradhi na vifo vya watu vinavyotokana na pombe hii feki

Mwisho ni wakati muafaka kwa viwanda halali kubuni muundo WA vifungashio ili mlaji aweze kubaini Kati ya feki na halali

Post a Comment

0 Comments

Close Menu