Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi ajira na vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete ameongoza Uzinduzi wa Maonyesho ya Ajira ya Nne (4) ya Tanzania na China yaliyofanyika katika Viwanja vya Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam , Jana . Maonyesho hayo ambayo yanalenga kutangaza na kuwaunganisha Vijana wahitimu na wenyeujuzi, Watanzania na makampuni ya Kichina yanayofanya kazi Nchini Tanzania.
Maonyesho hayo ambayo yanalenga kuwaunganisha vijana wa Kitanzania na fursa za Ajira, waziri Kikwete aliyafungua kwa kuwakumbusha umuhimu kuenzi ushirikiano uliopo wa nchi zetu mbili na hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan kutatua changamoto ya ajira nchini. Maonyesho haya yanataraji kutoa fursa za Ajira zaidi ya ajira 2000.
Mhe. Kikwete amesema maonesho hayo ni kati ya hatua za serikali ya Awamu ya Sita katika kutatua changamoto ya Ajira nchini, ambapo kupitia maonesho hayo makampuni ya China yanayofanya kazi hapa nchini yanaonesha mahitaji yao ya ujuzi wanaohitaji ili vijana wakitanzania weweze kuchangamkia fursa hizo. Hivyo vijana wenye sifa za mahitaji ya makampuni hayo kufuatia makubaliano baina ya serikali zetu katika kufikia maendeleo endelevu ambayo nchi yetu itafaidika katika shughuli za makampuni hayo nchini na kuwapa nafasi vijana wazawa wenye sifa wanazohitaji. Katika hatua nyengine nimewahakikishia watanzania kuwa serikali kupitia ofisi hiyo itaendelea kuratibu kwa tija masuala ya ajira nchini huku tukisimamia maslahi mapana ya Watanzania kqma ilivyoelekezwa nq sheria, sera na miongozo ya Ajira na Kazi na maono yq Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Comments