Blog Post

WAZIRI KIKWETE AKABIDHI VITI MWENDO NA FIMBO NYEUPE KWA WANAFUNZI CHUO CHA SABA SABA SINGIDA










Na Omary Mbaraka 

Hii sio kauli tupu bali ni vitendo kwa uongozi wa Awamu ya Sita ya Nchi yetu.Jana kwa niaba ya serikali Waziri wa kazi ajira na vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete amekabidhi Viti Mwendo na Fimbo nyeupe 100 kwa wanafunzi wanaosoma Chuo Cha Sabasaba, Singida. Shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Singida ni sehemu ya kutambua mchango wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Nchini ambao unasherehekea miaka 10 toka kuanzishwa kwake. 

Katika sherehe hizo Waziri Kikwete ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha kuwa Taasisi  hii ya WCF imefanikiwa sana katika miaka kumi ya utumishi. Na ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha pia katika miaka minne ya awamu ya sita (6) serikali imefanya mabadiliko ya sera na sheria  ambapo sasa fao jipya la utengemao limeanza hudumia watumishi wa umma wanaopata changamoto kazini. Lakini pia mfuko umefanikiwa kupandisha kima cha chini na juu ya pensheni ambapo sasa unalipa hadi shilingi Milioni 8.4 kutegemea aina ya fidia inayotakiwa kulipwa; kutokana na utendaji mzuri, taasisi imepata utambuzi wa ithibati ya kimataifa ya ISO ambapo ni ushuhuda kwa watumishi mabadiliko makubwa yaliyofanyika.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu