MAKALA
Na Omary Mbaraka
Kumekuwepo na MIGOGORO mingi ya ardhi ambayo huchukua muda mrefu kuitatua, mwingine ni kutoelewana kwa pande mbili za mgogoro,mingine huchelewa kutatuliwa kutokana na maafisa ardhi kuipuuza ama inakuwa ni mbinu zao katika kishawishi Cha kujipatia masilahi jambo ambalo vyote hivyo vinasababisha Taifa kukosa pato lake kutokana na ada mbalimbali ambazo zingelipwa
Ni muhimu kwa maafisa ardhi kuwa wazalendo kwa Taifa lao wakizingatia kuwa kuumaliza mgogoro wo wote wa ardhi atakuwa pia amelisaidia Taifa kupata pato lake kutokana na ada mbalimbali kama Kodi ya kiwanja,faini na fedha nyingi zikiwa ni ada mbalimbali zitakazo jitokeza wakati wa kuendeleza ardhi
Tukumbuke kuwa madhala ya kutokusanya fedha za ndani ndio kunapelekea mzigo mkubwa kwa Rais wetu kwenda nchi za nje kuomba mikopo
Ni wakati muafaka kwa watumishi mbali mbali wa serikali kutambua kuchelewa kwa mambo mbali mbali iwe baadhi za kesi mahakamani, migogoro ya ardhi nk ambazo zikitatulika mapema na serikali itapata fedha
Kwani niliwahi kushuhudia watu wawili waliokuwa wakilumbana na baadae kukubaliana wenyewe kuumaliza mgogoro wao lakini Bado maafisa ardhi waliendelea kuchelewesha wakidai Bado shauri Hilo linahitaji vikao mbalimbali ikiwemo kupitishwa mchoro na idhini ya wakubwa
0 Comments