Na Omary Mbaraka
Waziri katika ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na vijana na wenye ulemavu Mhe Ridhwani Jaksya Kikwete ameshiriki marathon ya Hisani iliyoandaliwa na Lions Club kuchangia fedha kwa ajili ya Uchunguzi na Tiba kutibu Uono Tanzania. Michango hii inakwenda kutumiwa kusaidia kufanya uchunguzi na kutibu Changamoto zinazotokana na magonjwa ya Macho.
Hii sio mara ya kwanza kwa Taasisi hii ya Lion’s Club kuchangisha pesa kwa ajili ya kusaidia wenye uhitaji. Wamekuwa wakisaidia tiba Nchini na rufaa za Nje ya Nchi pamoja na kusaidia programu mbalimbali za serikali kwa wenye uhitaji maalum ikiwemo watu wenye Ualbino, na Wenye shida ya Kuona kwa kutoa vifaa kama Fimbo Nyeupe na mashine za Braile.
0 Comments