Blog Post

HALMASHAURI ZA MIJI NA SERIKALI ZA MITAA ZIUNGE MKONO MAONO YA RAIS DKT SAMIA

                       MAKALA

Na Omary Mbaraka 

Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe dkt Samia Suluhu Hassan alikumbusha moja ya sheria au mikakati ya wizara ya Ardhi kuboresha miji mikubwa ya Tanzania ikiwemo Dar es salaam ,Dodoma, Mbeya ,Arusha, Kilimanjaro na Mwanza. Akitoa mfano kuwa utaona katika Barabara  kuu yamejengwa magorofa lakini nyuma yake Kuna nyumba zilizojengwa zamani zenye makazi duni

Kwa kuunga mkono jambo Hilo hivi majuzi tu waziri wa Ardhi Mhe Deo Ndejembi ameanzisha zoezi Hilo la kuboresha makazi kwa kuanzia jiji la Dar es salaam maeneo ya Msasani Mkangira

Hakika zoezi hili la kuboresha makazi na miundo mbinu linapaswa kuungwa mkono na wananchi na viongozi mbali mbali kuanzia serikali za mitaa,kata na Halmashauri za miji husika ili kupendezesha miji yetu na watu kupata makazi bora

Kuna masuala mengi yanayoweza saidia kuboresha makazi endapo nao wananchi wanapoamua kuboresha makazi yao kwa kufanya ukarabati kama vile kuondoa urasimu  wa upatikanaji vibali vya kukarabati nyumba zao badala ya kuwasimamisha kwa kuwapa "Stop order"ili walipe ada za ukarabati ni vizuri kuwaelimisha kulipa ada husika huku wakiendelea kuboresha makazi yao ikiwa ni njia moja wapo ya kuunga mkono wazo la RAIS wetu kuipendezesha miji yetu.

Kwani ni kweli pamoja na njia ndefu ya kufuata ili kibali kipatikane pia Kuna baadhi ya viongozi hutumia mwanya huo kujipatia masilahi na hivyo kibali kupatikana  kwa bei kubwa

Post a Comment

0 Comments

Close Menu