Blog Post

WIMBI LA UJENZI WA MAJENGO YASIO NA KIWANGO YAONGEZEKA

 Na Omary Mbaraka 

MAJENGO mengi yanayojengwa hivi karibuni hasa Dar es salaam hayana ubora hii ni kutokana na utafiti uliofanywa na chombo hiki Cha habari jambo ambalo upo uwezekano kuhatarisha maisha ya wananchi

Chombo hiki Cha habari kimetembelea MAJENGO mengi hapa nchini na kukuta MAJENGO yenye thamani kubwa zaidi ya milioni kumi hayajasajiriwa na bodi za ukandarasi CRB Wala ERB {Bodi ya uhandisi) hivyo baada ya uchunguzi wetu sababu kubw ni wajenzi wa MAJENGO hayo hawana usajili wa bodi hizo  kwa vile hawana sifai za kusajiliwa

Vile vile kwa Hali hio serikali inakosa mapato yakiwa ni kutokana na ada za usajiri na pia serikali inakoseshwa kuhakiki miradi hio ya UJENZI kama Ina ubora stahiki

Moja ya jengo la gorofa moja tulilotembelea ni Lile la kimara temboni ambapo tulipoongea na mhandisi wa jengo Hilo bw Mallya alikiri kuwa jengo Hilo halijasajiriwa na CRB Wala ERB pia alikiri hata yeye hajasajiriwa  na bodi ya uhandisi ERB


Post a Comment

0 Comments

Close Menu