Blog Post

WENGI WAMPONGEZA ASKOFU RWEYONGEZA ILI MANABII NA MITUME WABANWE

 Na Mwandishi wetu

Kauli ya askofu Rweyongeza ya kuitaka serikali ibane wimbi la manabii na mitume wanaozidi kujitokeza hapa nchini aliyoitoa katika jubilee ya askofu Rwoma katika Jimbo la katoliki Kayanga imeungwa mkono na wengi

Askofu Rweyongeza amesema ni wakati muafaka bunge na serikali kurekebisha ibara ya 19 (1) na (2) ya katiba yetu ya nchi ambayo inatoa uhuru wa kuabudu na kuhubiri dini na kufanya ibada kwa uhuru bila kuingiliwa na serikali matokeo yake wapo watu wamejitokeza na kujiita manabii au mitume bila uzioefu Wala kusomea wakiwa na malengo ya kujitajirisha,

Askofu Rweyongeza amekemea miujiza ya uongo ya kuwaponya watu na akasema kama kweli Wana uwezo waende katika ICU ya mahospitali wawaponye wagonjwa

Mwandishi wa habari pia amekutana na wananchi kadhaa ambayo wanaunga mkono kauli ya askofu Rweyongeza ambapo bw Jacob Ngaiza nae amesema  kama kweli hawa manabii Wana uwezo wangeenda muhimbili wodi ye yote kama vile Mwaisela wawaponye wagonjwa wote waliolazwa waondoke warudi majumbani bw J Ngaiza alisema watu wanaozidi kutiwa umasikini kwa kuwalaghai kutoa sadaka na kununua maji ama mafuta ambayo hayasaidii cho chote na baada ya kutiwa umasikini huo wanalaumu serikali ya mama dk Samia.

Nae  Eliza Christian amesema yupo nabii mmoja hakumtaja jina anakwenda mikoani kuwachukua watu na kuwafundisha jinsi ya kuwa walemavu na akifika katika mahubiri anajifanya kuwaondolea ulemavu huo na mlemavu wa ukweli asipoponywa anamusmbia Bado Hana Imani kubwa kwa mwenyezi mungu hivyo aongeze ibada

Hivi karibuni makamu wa Rais Dk Philip Mpango huko Arusha amemuagiza waziri wa mambo ya ndani kupitia idara ya usjiri kupitia vyema usjiri wa makanisa

Na hivi karibuni serikali ilifuta usajiri wa kanisa la Christian Life na miliki wa kanisa Hilo bw Dominic K Dibwe mzaire aliejiita Kiboko ya Wachawi kufukuzwa nchini 

Nae Imma Shango yeye anajiuliza kuwa serikali Ina vyombo vizuri vya ulinzi na upelelezi sijui inashindwaje kugundua udanganyifu mkubwa katika makanisa haya ambapo viongozi wake wamejilimbikizia Mali nyingi kwa udanganyifu



Post a Comment

0 Comments

Close Menu