Blog Post

WAKATI TUKIADHIMISHA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI LEO TUNALAANI PIA MAUAJI YA WAANDISHI WA HABARI HUKO GAZA

Mei 3 kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, ambapo uhalisia unaonesha hali ya Vyombo vya Habari si nzuri kimaudhui, kifedha, na kiteknolojia. Na ili kuepuka kufikia hali mbaya zaidi ni wazi kuwa Vyombo vya Habari vinatakiwa viwekeze kwenye teknolojia na waandishi kuongeza ujuzi, ili kuendana na wakati huku fedha ikitafutwa sambamba na serikali kuunga mkono kwa kuvipatia matangazo vyombo vyote vya habari kwa usawa kwani ni ukweli kwamba asilimia 80 ya mapato ya vyombo vya habari hutokana na matangazo. Aidha, sote tunatambua ujio wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka huu 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025, katika hili Vyombo vya Habari vinatakiwa kutoa nafasi sawa kwa vyama vya siasa katika kuripoti matukio mbalimbali. Nchini Tanzania maadhimisho haya pia yanafanyika na kwa siku ya kwanza Spika wa Bunge, Tulia Ackson alikuwa mgeni rasmi na alikazia kwa kusisitiza ufuatiliaji wa taasisi za serikali zinazodaiwa fedha na vyombo vya habari, ili walipe madeni yao na vyombo viweze kujiendesha. Leo Mei 3, 2024 ni kilele cha siku hii muhimu kwetu, mgeni rasmi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, tunataraji kuna jambo ataliongea ingawa tayari Waziri mwenye dhamana ya Habari Nape Nnauye amesema jambo. Namnukuu, “hali ya uhuru wa vyombo vya habari katika nchi yetu inaendelea kuimarika, hatujafika tunakotaka kwenda lakini kwa hakika hatupo tulipokuwa jana, mazingira ya jana na leo ni tofauti na wanahabari wanakubaliana na mimi, tumefika hapa kwenye maboresho haya yaliyofanyika kwa sababu ya utashi wa kisiasa wa serikali.” Pia katika siku hii ya kuadhimisha uhuru wa habari Tafakari news Weblog inalaani vikali mauaji ya waandishi wa habari wapatao ishirini na mbili na wengine kushikiliwa na majeshi ya Israel katika vita vinavyoendelea Gaza

Post a Comment

0 Comments

Close Menu