Blog Post

ONDOENI WASIWASI NCHI IMEHIFADHIWA VIZURI - KIKWETE




Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwan Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wahifadhi Kumbukumbu alipotembelea kuona maandalizi ya mkutano mkuu wa chama hicho jijini Dodoma hivi karibuni.

Na MWANDISHI WETU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofis ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwan Kikwete, amewatoa wasiwasi watanzania kwa kuwa nchi iko salama na  imehifadhiwa vizuri. 

Mhe. Ridhiwan alisema hayo baada ya ziara ya Kamati ya kudumu Bunge inayosimamia Utawala , Katiba na Sheria kutembelea idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa , Dodoma. 

Akizungumza mbele ya kamati Mhe.Ridhwani, pamoja na kuishukuru kamati kwa kufanya ziara ameeleza kuwa ofisi yake itasimamia na kutekeleza maelekezo yote kwa kuwa tayari Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika Idara hiyo na mrejesho utatolewa kwa mujibu wa utaratibu mapema iwezekanavyo.

“Ujio wenu hapa umeambatana na maelekezo muhimu sana kwetu ili kuimarisha shughuli zinazofanywa na Idara hii kwa ustawi wa Serikali na Taifa kwa jumla, nasi tuko tayari kutekeleza maelekezo hayo kwa haraka na ufanisi,” alisema Mhe. Kikwete.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Dkt. Mhagama amemsisitiza Naibu  Mhe. Ridhiwani kuhakikisha ofisi yake inasimamia vyema Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa katika zoezi la kuhifadhi nyaraka ambazo zimekusanywa hivi karibuni ili ziwe kwenye utaratibu mzuri kama zilivyo nyingine kwa lengo la kuepuka upotevu wowote wa nyaraka hizo.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu