Wakazi wa Zanzibar, watalii na wageni kutoka nje ya visiwa vya Zanzibar wakati wa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wanatarajia kupata burudani ya kukata na shoka katika hotel maarufu iliyoko visiwani Zanzibar ya Cterra.
Kwa mujibu wa viongozi wa hoteli hiyo burudani zilizoandaliwa wakati wa msimu huu wa siku kuu za Christmass na mwaka mpya hazijawahi kutokea ndani ya hotel hiyo na visiwani kwa ujumla.
Wamejipanga kuhakikishia kuwa unapata burudani na kuifanya siku zako za mwisho wa mwaka zinakuwa ni maalum na za kipekee, kukupa burudani ya aina yake.
Kutakuwa na live bendi kali zitakazotumbuiza na densi show katika siku ya siku kuu watoto wote chini ya miaka mitatu watapata chakula bure, watoto chini ya miaka 12 walipa dola 20 na watu wazima watalipa dola 40.
Bila kuhasau michezo ya pool, na ile ya ufukweni mwa bahari pamoja christmass tree zitapambwa katika siku za siku kuu.
0 Comments