Blog Post

BIASHARA MTANDAONI INAZIDISHIKA KASI, JIFUNZE JINSI YA KUNASA WATEJA

Best designer shopping outlets - including where to bag the biggest  discounts | The Sun

Na IBRAHIM KADILO

Kabla ya kuamua kurusha tagazo lako kwenye mitandao ya kijamii, unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi ili kuweza kufanikisha kufanya mauzo mtandaoni kwa urahisi zaidi bila kutumia nguvu nyingi.

Katika makala haya ntakueleza jambo moja la msingi sana kabla ya kurusha tangazo lako unalotakiwa kuzingatia katika biashara yako ni kuchagua walengwa wako sahihi wenye matatizo sugu yanayosumbua.

Kabla ya kuendelea mbele nieleze kwa ufupi target market ni nini? Hili ni kundi fulani la watu wenye mahitaji yanayofanana, mfano fikiria upande wa afya na urembo, hili ni eneo pana sana katika soko, saloon ya urembo inaweza kutoa huduma za aina mbalimbali.

Kama vile kukata kucha, kufanya make up,  massage nk. Kwa mfano tukichukua moja katika ya huduma hizo za saloon kama kufanya massage.

Hiyo ndio linakuwa target market yetu au kwa jina lingine ndio niche yetu tunaweza kuongeza zaidi kujipambanua kwa kutoa massage kwa wanaume.

Hilo ni kundi la watu ulilolipambanua vizuri unaweza kufikiri kwa nini tunajiweka kizuizi kwenye soko kwa sababu fedha zetu za kufanya marketing hazitoshi kama utalenga soko pana zaidi ujumbe wa kuwafikishia walengwa wako utakuwa dhaifu.

Pia lengo la matangazo yako ni kwa walengwa wako (prospects), ili kuona tangazo lako na kusema “waoo hili ni kwa ajili yangu”

Hii ndio maana unahitaji kuchagua soko lako lengwa kwa kuwa kila kitu kwa kila mtu inapelekea suala zima la marketing kushindwa kufanya kazi.

Hii haimaanishi huwezi kutoa huduma kwa wengini, elewa kuwa tunajiainisha na huduma lengwa kwa ajili ya kufanya kampeni katika marketing iwe rahisi.

Kujaribu kumlenga kila mtu inamaanisha kuwa haujamlenga mtu yeyote, kwa kuwa na soko pana unaua namna ya kujitofautisha na washindani wako na hivyo kuua kabisa mkakati wa masoko.

Jinsi ya kuchagua walengwa wako?

Baada ya kuelewa umuhimu wa kuchagua target market kabla ya kurusha matangazo yako kwenye mitandao ya kijamii, sasa ni wakati wa kuchagua soko lako lengwa, ebu tuangalie mfano wa mpiga picha anavyoweza kuchagua soko lake lengwa.

Mpiga picha anaweza kuwa anatoa huduma za kupiga picha za harusi, picha za makampuni, picha za waandishi wa habari, picha za familia, hii ni aina pana sana ya soko la picha. Njia nzuri ya kufikiria jinsi ya kuchagua soko lako lengwa ni kutumia kanuni ya PVP Index.

PVP index  ni ( Personal fulfillment, Value to the marketplace and Profitablility),  yaani katika kanuni hii unaangalia Kulidhika kwako wewe binafsi kwa kutoa huduma hiyo kwa kundi la watu fulani, kuna watu huwa wanafanya kazi wasizozipenda kwa sababu ya fedha.

Personal fulfillment unaangalia kiwango cha kulidhishwa kwako kutoa huduma hiyo, kiasi gani unafurahi kushughulika na hao watu.

Value to the marketplace, unafanya tathimini ya huduma hiyo unayotoa kwenye soko hilo kwa kiasi gani soko hilo linathamini kazi yako.

 Profitability unaangalia kiwango cha faida kwa kutoa huduma hiyo kwenye soko kinalidhisha ni chenye faida.

Kwa mfano mpiga picha anaweza kuchagua soko lake lengwa  kama ifuatavyo:

Kwa kutoa huduma ya kupiga picha za harusi Personal fulfillment akajipa alama 5, Value akajipa alama 7, kwenye profitability akajipa alama 9 jumla ya alama 21.

Kwenye kutoa huduma ya picha za makampuni Personal fulfillment akajipa alama 3, value akajipa alama 6,  profitability akajipa alama 9 jumla ya alama 18.

Kwenye kutoa huduma ya picha za waandishi wa habari Personal fulfillment akajipa alama 9, value alama 7, profitability  alama 2 jumla  ya alama 18.

Kwa kutoa huduma ya picha za familia Personal fulfillment akajipa alama 9 value akajipa alama 8 na profitabilty akajipa alama 9 jumla ya alama 26.

Hapa  walengwa wa mpiga picha huyu ni wale wanaohitaji picha za familia kwa sababu ndio kazi anayoifurahia yenye faida na inathamani kubwa kwenye soko kuliko zingine.

Hii haimaanishi kuwa huwezi kushughulikia soko lingine bali juhudi zetu za kufanya masoko zitajikita kwenye soko letu lengwa zaidi.

Punde tutakapo dhibiti soko hili ndio tunahama kwenda kwenye soko lingine hivi ndiyo unaweza kuchangua soko lengwa na kufanikiwa katika kufanya mauzo mtandaoni. 

Kupata mafunzo zadi ya bure ya jinsi ya kufanya biashara mtandaoni tuma ujumbe whatsapp namba  0744499499 utaunganishwa kwenye group la whatsapp.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu