Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka, jiji Dodoma alipokuwa akikagua maandalizi ya mkutano wa chama hicho.
Wanachama wa Chama cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka wakimsikiliza Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa, jiji Dodoma kukagua maandalizi ya mkutano wa chama hicho.
Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akisalimiana na viongozi Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka, jiji Dodoma alipokuwa akikagua maandalizi ya mkutano wa chama hicho.
Na MWANDISHI WETU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete, amewataka viongozi wa Chama cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Ridhiwan aliyasema hayo jijini Dodoma alipohudhuria na kukagua maandalizi ya mkutano Mkuu wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka unaotarajia kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa, Oktoba 27, mwaka huu.
Pamoja na kukagua maandalizi ya mkutano huo, Naibu Waziri Ridhiwan Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwasalimia wanachama wa Chama hicho na kuwatakia uchaguzi mwema.
Katika salamu zake ,Mhe. Naibu Waziri aliendelea kuwakumbusha kazi nzuri zinazofanywa na serikali ikiwemo kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili hususani zile za kimuundo, kupanda madaraja, kubadili kada nk.
Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwa siku nne jijini Dodoma utahitimishwa na uchaguzi wa viongozi wa Chama hicho.
0 Comments