Blog Post

NI MARUFIKU KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII'


Na Mwandishi Wetu


SERIKALI imeonya kuhusu matumizi ya nyaraka za Serikali kupitia mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo imetolewa  na Naibu Waziri wa Nchi Menejimenti ya  Utumishi Wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoani Dar es Salaam Janejelly James  Ntate , Bungeni Dodoma .

Mh. Kikwete aliwakumbusha Bunge na wananchi kwa jumla kuwa mawasiliano serikalini yanasimamiwa na sheria na kanuni hivyo ni muhimu kwa wananchi kuzingatia taratibu hizo ili sheria zisiwabane na kuleta taharuki isiyokuwa ya msingi. 

Kufuatia kauli hiyo ya Serikali, Mbunge wa Viti Maalum Sophia Hebron  Mwakagenda kutoka mkoani Mbeya akataka kujua ni jinsi gani serikali imejipanga kwenye ujenzi wa mifumo hasa ukizingatia teknolojia ndiyo inakwenda kwa haraka sana. 

Akijibu swali hilo , Naibu Waziri Kikwete alieleza kuwa wazi imeendelea kujenga mifumo mbalimbali ya tehama na uwepo wa sheria Namba 10/2019 umewezesha serikali kuwa na uhalali wa uundaji wa mifumo hiyo na hadi sasa mifumo mbalimbali imejengwa kusaidia mawasiliano serikalini na kurahisisha uchapaji kazi.



Post a Comment

0 Comments

Close Menu