Na Mwandishi Wetu, CHALINZE
HALMASHAURI ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani,
wamepokea gari la Zimamoto na Uokoaji punde yanapotoke majanga hayo wilayani
hapo toka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (SSF) Jenifa
Shirima.
Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Chalinze,
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete amemshukuru Mrakibu Mwandamizi
huyo kwa niaba ya serikali kwa kuona kuwa katika mipango ya serikali Chalinze
nayo iwe moja ya maeneo ya kipaumbele katika uhitaji wa gari hilo.
Mbunge
alikumbusha kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Chalinze na majanga yaliyowahi
kuwakuta na kusema ujio wa gari hilo ni ukombozi mkubwa.
Akizungumza kabla ya kumkabidhi Mbunge wa jimbo
hilo, Mrakibu Mwandamizi Jenifa alimpongeza Mbunge kwa kuwasemea wananchi wake
na kusema gari hilo ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge Kikwete.
Mrakibu alimuahidi Mbunge huyo ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora kuendelea kutatua kero za zimamoto
katika halmashauri zote mkoa na kwamba na pia kumshukuru Mkurugenzi mtendaji wa
Chalinze kwa kuwapatia Kiwanja ambacho watajenga Jengo la zimamoto la wilaya na
ofisi zao.
Pia alimuhakikishia Mbunge kuwa serikali
inajipanga kwa ajili ya ujio wa gari kubwa wilaya hiyo.
Wananchi wa Chalinze kwa jumla yao wameishukuru
Serikali kwa kutatua kero hiyo ya muda mrefu na Wameahidi kulitunza gari hilo.
0 Comments