NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameshiriki katika mazishi ya
Marehemu Bi. Khadija Abbas Rashid aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya
udongo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1965, ambaye
amefariki tarehe 22 Agosti, 2023 Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu
(Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi ameshiriki pamoja
na Kaimu Mkurugenzi wa Idara Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa
Selengu katika shughuli hiyo.
Marehemu Bi. Khadija alizaliwa tarehe 23 Oktoba, 1949 na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Wasichana ya Forodhani - Unguja, ameacha watoto tisa.
0 Comments