MAFANIKIO HAYA NI MATOKEO YA KAZI KUBWA NA USHIRIKIANO, TUSIBWETEKE.
Mwalivundo, Chalinze
Akiwa ziarani katika kijiji Cha Mwalivundo, aliwashukuru wananchi wa kata ya Pera na Halmashauri ya Chalinze kwa ushirikiano na kazi kubwa inayoleta matunda makubwa, Nguvu ya wananchi
Baada ya ziara na ukaguzi wa miundombinu Mhe Ridhiwani Kikwete alipata wasaa wa kuzungumza na wananchi na kuwaeleza kuwa ameridhishwa na maendeleo yaliyofanyika na kuwa haya ni matokeo mazuri ya ushirikiano baina ya wanajamii.
Mhe Ridhwani Kikwete pia aliishukuru Serikali chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa fedha za miradi zilizochangia ujenzi huu wa madarasa matano na vyoo katika shule ya msingi Mwalivundo, ambayo ilikuwa kwenye hatari ya kufungwa kutokana na ukosefu wa madarasa na vyoo vyenye ubora. Leo shule imekamilika na watoto wanakwenda shule bila kuwa na changamoto zozote! Kwani huduma zote muhimu za kijamii zimeboreshwa ndani za viwango.
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete anaendelea na ziara yake jimboni kwake
0 Comments