*CHONGOLO: "UWEKEZAJI KWENYE BANDARI UNAYO TIJA, HATUWEZI KUTETEA JAMBO LISILOFAA KATIKA NCHI YETU"*
🇹🇿 *KOMBORA* 🇹🇿
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewaambia wananchi wananchi kwamba uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam hawatarudi nyuma kwa kuwa una tija kubwa kwa Watanzania.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohusisha wananchi wa kanda ya kaskazini ikijumuisha Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Julai 22,2023, Chongolo amewaomba wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa ina kazi kubwa ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo.
Akizungumzia faida za uwekezaji utakaofanyika bandari ya Dar es Salaam, amesema nchi itapata faida kubwa kwenye kodi ambayo itakwenda kwenye miradi mbalimbali kutatua changamoto za wananchi.
Amesema Chama Cha Mapinduzi hakiwezi kutetea jambo ambalo halipo sawa kwa sababu kinajua wananchi wanataka nini na ikifika wakati wa kuomba kura lazima warejee tena kwao.
" Tunasema haya tukiwa na nguvu tukiwa kifua mbele kwamba jambo hili linatija kwa nchi, lina tija kwa maendeleo ya nchi na tuliahidi wenyewe na kwa hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na sisi ni sehemu ya Watanzania.
Chongolo amesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam lengo kwa ujumla wake linalenga kuongeza tija , kwani kwa sasa kiwango kinachokusanywa kwa asilimia 99 kinatumika pale pale kwenye uendeshaji.
🇹🇿 *KOMBORA* 🇹🇿
0 Comments