Blog Post

TULINDE AMANI KWA KUMKUMBUKA MWENYEZI MUNGU



Na Ismail Mang'ola 


Mwenye Kiti wa hifadhi ya Makaburi ya Jumuiya ya Mabohora jijini Dar es Salaam ameitaka jamii kuilinda amani iliyopo pamoja na kumkumbuka Mwenyezi Mungu ili aweze kunusuru vile vinavyojitokeza na kuleta madhara kwa jamii na taifa kwa ujumla.


Amesema Kuna haja Pana kuilinda amani iliyopo hapa Tanzania na duniani kwa ujumla kwani kumekuwepo na mambo mengi ambayo yanaviashoria vya kuvuruga amani iliyopo na kuitaka jamii kuhakikisha wanavishinda vita hivyo vyenye athari ya uvunjifu wa amani tunayotamba nayo.


Hayo yamesemwa na Makamo Mwenyekiti wa uhifadhi wa Makaburi ya Jumuiya ya  Mabohora, Sheikh Mudhaifa Seifuddin Jamal Simba wakati wa kusheherekea sikukuu ya Eid-El Adha 'siku ya kuchinja' iliyofanyika katika makaburi ya Mabohora Upanga jijini Dar es Salaam.


Sherehe hizo za Eid Al-Adha ambazo zimefanyika duniani kote,  Mudhaif amesema, viongozi wa dini pamoja na taasisi zingine zinapigania kuwepo kwa amani waendelee kulipambania taifa, kwani iwapo kama ulinzi huo wa amani hautasimamiwa vyema hivyo hakutakuwa na Ibada, wala suala la kuchinja kuchinja na kusherehekea siku kuu ya aina yeyote.


Amesema muendelezo wa Jumuiya hiyo kwa kuchinja, mwaka huu umekuwa na changamoto kidogo kwani hata gharama za mbuzi na kondoo zimekuwa juu mno tofauti na miaka mingine.


Amebainisha kuwa, msimu huu mbuzi Mmoja amenunuliwa kwa shilingi 260,000 tofauti na misimu iliyopita ambapo mbuzi aliuzwa kwa bei ya 170,000 Hadi laki mbili huku bei ya kondoo nao wakiuzwa kwa bei tofauti kidogo na mbuzi.


Mudhaifa amesema idadi ya mbuzi walionunuliwa ni 260 na kondoo 217 ambao wote wamechinjwa.



Post a Comment

0 Comments

Close Menu