Na Omary Mbaraka
Moja ya Taasisi nyeti ya Chama Cha Mapinduzi Jitegemee trading co ltd zamani ikijulikana Sukita imejikuta ikiingia katika mzozo mkubwa na wapangaji wake na hatarini kudaiwa mabilioni ya shilingi.
Jana tarehe 5 Julai 2025 katika kiwanja nambali 1010/1 Buguruni industrial area karibu na Barabara ya Mandela Mwandishi wa habari hizi alishuhudia Bulldozer kubwa likitoa Mali iliohifadhiwa katika kiwanja hicho na kuwekwa nje ya uwanja huo
Tulipo ongea na askari wa Suma JKT waliopo katika eneo la tukio walisema eneo Hilo limepangishwa kwa mtu mwingine na hivyo Jitegemee trading co ltd ilitoa notisi ya siku saba ili wapangaji wa awali ambao ni Badri East African Enterprises Ltd na Ital African Limited watoe Mali zao na wakasema hapa nje watazilinda kwa siku saba tu
Pia tulifanikiwa kufika na kuongea na uongozi wa kampuni ya Badri East African Enterprises ambao walikili zile ni Mali zao ambazo zina thamani ya T shs bilioni 22 na wao mpaka hivi Sasa Wana miaka 25 ya upangaji katika eneo Hilo na hapo awali kulikuwa ni kiwanja tu lakini wao ndio wamepaendeleza kuzungusha ukuta na kujenga jengo la ofisi kama linavyoonekana katika picha tulizoambatanisha Hivyo basi walisema uongozi wa Jitegemee trading co ltd haukutumia busara kwani wao Bado ni wapangaji na waliwaomba kukaa mezani KUTATUA changamoto hivyo wanachofanya ni kinyume Cha sheria na wanahofia Mali zao nyingi kupotea
Uongozi huo ulisema katika uwanja huo Kuna makontena 19 za futi 20 na makontena 10 ya futi 40 ambayo yamehifadhi spea mbalimbali za vifaa vinavyotumika miradi ya ujenzi wa Barabara nk kama vile injini, gearbox,seti za spring, deaf pia Kuna magari ,na Bulldozer nk vyote vina thamani ya bilioni 22 ambazo zipo hatarini kuibiwa na hivyo kulitia hasara Taasisi ya CCM kuwajibika kulipa
Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa pia kupata nyaraka kadhas na picha ambazo zimeambatanishwa hapa zinazo onyesha kampuni ya Badri East African Enterprises ni wapangaji halali na mwaka 2022/2023 walilipa milioni 30.Juhudi za kumpata mkurugenzi wa Jitegemee trading zinaendelea
0 Comments