Blog Post

WAZIRI KIKWETE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAAJIRI (ATE)







 Na Omary Mbaraka 

Waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete alifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Cha Waajiri (ATE) mjini Dar Es Salaam tarehe 18 Juni 2025 ambao umekuwa wa mafanikio makubwa sana.

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na taarifa za kiutendaji za mwaka na kongamano kujadili mabadiliko ya sheria za kazi na athari yake kwa Waajiri na Waajiriwa katika kuleta Tija. Nimepata nafasi ya kushiriki na kusikia mafanikio na changamoto zilizomaliza na haswa hali ilivyokuwa kabla na baada ya mabadiliko ya sheria. 

Nimetumia Mkutano huo kueleza  nafasi ya serikali katika Utatu wa mashirikiano baina ya wadau wakuu watatu wa Kazi. Katika hotuba yangu nimeeleza nia ya mabadiliko hayo na kuwashukuru sana ATE kwa ushiriki wao katika kuhakikisha tunakuwa na sheria nzuri za kazi na kusimamia utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya Kimataifa ya Wafanyakazi ambayo Tanzania ni Mwanachama wa Mikataba hiyo.

Pia nilitumia nafasi hiyo kuwashukuru sana wadau wetu wa maendeleo shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa kuendelea kushirikiana nasi na pia kuwapa salamu za hongera toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa ILO Cde. Gilbert F. Houngbo.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu