Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Nchi ya Uswisi nchini Tanzania, Nicole Providoli, Ofisini kwake, iliopo jijini Dar es Salaam Mei 16, 2025 alipofika kujitambulisha.
Katika kikao hicho, Mhe Kikwete alimshukuru Ndg. Balozi kwa ushirikiano uliodumu wa zaidi ya miaka 63 baina ya nchi zetu mbili na kumuhakikishia kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua mchango mkubwa wa Serikali ya Uswisi kupitia shirika la Swiss Aid na ushirikiano unaoendelea katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, maendeleo ya jamii pamoja na masuala ya ukuzaji ujuzi kwa vijana.
Kwa upande mwingine Mhe Kikwete alimpongeza na kuushukuru ubalozi wa Uswisi kwa mchango wake katika kufanikisha kukamilika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana (2007), Toleo la Mwaka 2024 ambayo inatoa mwongozo kwa vijana na wadau wengine kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi; na utayari wao kusaidia usambazaji wa Sera hiyo kuwafikia Wadau.
0 Comments