Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China ukiongozwa na Balozi wa China Nchini Balozi Chen Mingjian Ofisini, Dodoma.
Katika kikao hicho
Balozi Mingjian alitumia wasaa huo kujitambulisha na kuendelee kuimarisha ushirikiano wa China na Tanzania, alikumbusha maeneo muhimu ya ushirikiano haswa mahusiano baina katika mafunzo ya kujenga ujuzi na ufundi huku msisitizo mkubwa ukiwa kuwaandaa vijana watakaopambana na mabadiliko makubwa ya kidunia hasa katika mapinduzi ya Teknolojia.
Kwa upande wake Mhe Kikwete amewahakikishia kuwa Nchi yetu ya Tanzania itaendelea kuenzi uhusiano uliopo baina ya nchi zetu na kuwa tutaendeleza uhusiano huu kwa kuimarisha maeneo yote ambayo yanatukutanisha katika mashirikiano haya. Pia aliishukuru serikali ya China kwa mabadiliko makubwa ambayo yanaelekea kukuza ujuzi kwa vijana wa Kitanzania na nia yao ya kufanya maonyesho makubwa ya Kazi yanayolenga kufunua fursa za vijana wa kitanzania kujiajiri na kufungua milango ya kuajiriwa na makampuni makubwa ya kigeni yakiwemo ya China nchini hapa. Alisema waziri Kikwete
0 Comments