Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi, ajira na vijana, na wenye ulemavu katika ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jaksya Kikwete ametangaza kuwa MBIO za mwenge kwa MWAKA huu wa 2025 zitaanza siku Jumatano Tarehe 2/04/2025 katika uwanja wa shirika la elimu kibaha
Na kauli mbiu ya mwaka huu ni"Jitokeze kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025 alisema waziri Kikwete. Hivyo basi aliwaomba na kuwakaribisha wananchi wote kuja kushiriki tukio muhimu la kuwasha mwenge wa Uhuru ikiwa ni ishara ya kuanza Rasmi kwa Mbio za Mwenge utakao zunguka katika Mikoa 31 Halmashauri 195 Nchini Kwetu. Nyote Mnawakaribishwa.
Waziri Kikwete alikumbusha kuwa kwa mara ya kwanza Hayati mwalimu Julius Nyerere aliwasha mwenge tarehe 9 desemba 1961 ambapo alisema maneno makubwa kuwa "tumekwisha washa mwenge na tuuweka juu ya mlima Kilimanjaro umulike ndani na nje ya mipaka yetu na ulete mafanikio pale ambapo hakuna matumaini na ulete upendo mahali penye chuki na heshima mahali palipojaa dharau"
0 Comments