Blog Post

CCM ILIACHIA NJIWA 500

 Na Omary Mbaraka 

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeadhimisha miaka 48 tangu kuanzishwa kwake katika mji mkuu wa taifa wa Dodoma, kwa kuachia njiwa 500 kuashiria dhamira yake ya kuleta amani na utulivu ambayo nchi imekuwa nayo kwa miaka mingi.

“Kwa niaba ya wenyeviti wote wa CCM wa mikoa, tunawatoa njiwa hawa ikiwa ni ishara ya amani na umoja unaotambulisha taifa letu,” alisema Adam Kimbisa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.

Akihutubia wanachama na wafuasi wa CCM waliokusanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Kimbisa alimmwagia sifa kemkem Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na mchango mkubwa katika kuleta maelewano na kuhakikisha utulivu nchini kote.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla alisema chama tawala kimeweka misingi imara ya umoja wa kitaifa na kitaendelea kuenzi mirathi yake.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi, alisisitiza dhamira ya chama hicho kufanya uchaguzi mkuu wa haki na huru Oktoba mwaka huu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Mpango, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira, pamoja na viongozi wengine.



Post a Comment

1 Comments

  1. Nawapongeza kwa kuandaa habari mbalimbali za Kijamii, mungu awabariki TAFAKARI NEWS WEBLOG

    ReplyDelete

Close Menu