Blog Post

WAZIRI AKAGUA KITUO CHA MKONGO WA TAIFA BAHARINI

 


Na Omary Mbaraka 

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea na kukagua  Kituo Cha kupokea Mkongo wa Taifa kutoka  Baharini kinacho milikiwa na Kampuni ya SEACOM kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam  Januari 6,2025.

Aidha, Mhe Mahundi amesema lengo la kutembelea Kituo hicho kinacho pokea Mkongo wa Taifa kutoka Baharini  ni kujiridhisha kama miundombinu iliyopo inajitosheleza kuendelea kutoa huduma ya Mawasiliano kwa Watanzania.

Katika Ziara hiyo Mhe Mahundi ameambatana na Mhandisi Secili Francis ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi kutoka katika Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL) pamoja na wataalamu wengine kutoka TTCL na Kampuni ya SEACOM.

Hivi karibuni Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha Mawaziri wa Wizara hiyo alisema lengo la kutenganisha Wizara hiyo na ya Habari ili kuleta ufanisi mkubwa zaidi kuboresha mawasiliano na kuongeza fursa za kiuchumi

Post a Comment

0 Comments

Close Menu