Taarifa kutoka Korea Kusini zinaeleza kuwa Polisi na wapelelezi wa kupambana na rushwa wamefika kwenye makazi ya Rais Yoon Suk Yeol jijini Seoul ili kutekeleza agizo la kukamatwa kwake.
Rais huyo anatakiwa ili kuhojiwa kuhusiana na tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kuongoza uasi, kosa ambalo hukumu yake inaweza kuwa kifungo cha maisha au hata adhabu ya kifo.
Hivi karibuni kwa mara 3 tofauti Rais Yeol alikataa wito kutoka kwa wapelelezi.
Jumanne wiki hii Mahakama nchini humo ilitoa hati ya kumkamata, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hati hiyo kutolewa dhidi ya Rais aliye madarakani.
Taarifa za awali zinasema kuwa zoezi la kumkamata Rais huyo ambaye “amesimamishwa/kuvuliwa mamlaka” linazuiliwa na kitengo cha kijeshi.
❇️Endelea kuifatilia #UkomboziNews kwa taarifa zaidi
0 Comments