Na Omary Mbaraka
Tukio la kusikitisha lilitokea tarehe 6 oktoba 2024 maeneo ya segerea chama shina namba 18 ambapo bi Vailet Castor Lumato maarufu mama mchungaji alipo mmwagia uji WA moto aliekuwa mke mwenza bi Alfreda Ndunguru na kujeruhiwa vibaya na hatimae kukimbizwa katika hospitali ya mkoa Amana iliopo ilala Dar es salaam
Tukio Hilo liliropotiwa kituo Cha polisi Stakishari ambapo mama mchungaji alikuwa akishikiliwa na jeshi la polisi huku wakifanya uchunguzi
Hivyo basi Leo hii mama mchungaji amefikishwa katika mahakama ya wilaya Kinyerezi akisaidiwa na wakili wake na hivyo kuachiwa kwa dhamana
Inadaiwa bi Alfreda Ndunguru aliitwa na watoto wake kuuguzwa katika nyumba ya mtalaka wake jambo ambalo mama mchungaji hakupendekezwa na hivyo alichemsha uji na ilipofika saa tano na nusu usiku wakati bi Alfreda amelala alimwagiwa uji na kujeruhiwa vibaya
Chombo hiki Cha habari kilifika hospitali ya Amana ambapo kilikutana na afisa mahusiano mmoja wapo bw Mndolwa na kuthibitisha ni kweli bi Alfreda Ndunguru amelazwa wodi ya "private"na hivyo tunaendelea na uchunguzi kujua kisa na pia kuona jinsi Gani bi Alfreda alivyojeruhiwa na anaendeleaje na matibabu
0 Comments