Na Anania Njonjo na Omar Mbarak
Kampuni ya Prime Machinery Ltd iliopo eneo la Kipawa Ilala Dar es Salaam, imegushi nyaraka ya serikali kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Nchini (TPHPA), iliyoko chini ya Wizara ya Kilimo.
Nyaraka hiyo kutoka wizara ya Kilimo (Phytosanitary Certificate), ambayo inatolewa kama uthibitisho kwa mteja anayepokea mzigo, na hutolewa baada ya mzigo kusafirishwa.
Kwa mujibu wa nyaraka hiyo kutoka kwenye chanzo cha habari cha kuaminika ndani ya kampuni hiyo, ilitumika kusafirisha ufuta magunia 1,059 kwenda kwenye kampuni ya GS SETHI & SONS iliopo Mumbai India.
Nyaraka halisi kutoka TPHPA inaonesha shehena hiyo ya ufuta ulifanyiwa upulizaji wa dawa kuua wadudu tarehe 3 julai mwka huu, wakati ile iliyogushiwa kusafirisha ufuta huo inaonyesha ufuta huo ulikuwa ulifanyiwa upulizaji wa dawa 22 julai mwaka huu.
Pia katika nyaraka hizo zinaonyesha kuwa uongozi husika TPHPA uliidhinisha na kusaini tarehe 15 julai mwaka huu, lakini cha kushangaza nyaraka iliyogushiwa inaonyesha upulizaji wa dawa umefanyika baada ya kuidhinishwa kuondoka 15 julai mwaka.
Hata hivyo waandishi wa habari hizi walikutana na kizaa zaa kikubwa baada ya uongozi wa kampuni hiyo ya Prime kukataa kutoa ushirikiano.
Uongozi kampuni hiyo bila kujibu hoja za kugushi nyaraka hiyo walijitapa kuwa wao wana uhusiano mkubwa na Jeshi la polisi.
Pia, walizidi kutishia waandishiwa wa habari kuwa watawaita polisi ili wawatie nguvuni.
Katika hali ya kushangaza alijitokeza mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Benjamini ambaye alionekana kama msemaji wa kampuni hiyo.
Hata hivyo, Bw Benjamini alishindwa kujibu hoja ya kughushi nyaraka.
Alizidi kuwatisha waandishi wa habari hizi kuwa kamera za ofisi zinawachukua huku akidai kuwa mali hio ya ufuta iliyosafirishwa ilikuwa Bw Seti wa Kampuni ya IPTL.
Bw Benjamini alijitapa kuwa yeye kapelekwa hapo kwenye hiyo kampuni na marehemu hayati John Magufuli akitokea jeshini.
Afisa mmoja mwandamizi wa TPHPA, ambaye hakutaka kujitambulisha alipoulizwa kuhusu nyaraka hiyo iliyogushiwa alikiri kuitambua nyaraka hiyo, japokuwa kilichoandikwa kilikuwa tofauti.
Akijibu hoja ya kugushi nyaraka za TPHPA, afisa mkuu wa kampuni ya uwakala wa forodha ya Tricon alipozungumza kwa njia simu alijibu kwa ghadhabu kuwa suala hilo lifuatiliwe Wizara ya kilimo.
Blog hii inaendelea kuchunguza kampuni nyingine mbili zilizohusika katika kusafirisha ufuta huo ya Gallas na Fairways.
0748881303
0 Comments