Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati Singida, Dkt. Cyprian Hilinti amemuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aridhie kuitwa Mama wa Taifa kwakuwa ni Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania, kama ambavyo Rais wa kwanza Mwanaume Mwl. Julius Kambarage Nyerere alivyoitwa Baba wa Taifa.
Akiongea mbele ya Rais Samia kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mkoa wa Singida tarehe 16 Oct 2023, Askofu Hilinti amesema “Mama sisi wa Singida tunakushukuru unaleta fedha kama ilivyotajwa na RC, unafadhili miradi mbalimbali, sisi Viongozi wa Dini tunakuhakikishia usiogope kelele za mamba, fanya kazi na sisi tunakuombea usiogope vibwengo na vinyamkera vitashindwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti” “Na Mungu atakusaidia Mama utamaliza vipindi, sio kipindi, vipindi vyako salama, kazi zako zinakutangaza, zinakupigia kura siku ile sisi tutakuwa tunachovya wino na kuweka dole.
Jambo la mwisho Mh. Rais, tulikuwa na Rais wa kwanza Baba (Mwl. Nyerere), tukampenda tukamuita Baba wa Taifa, sasa tunaye Rais wa kwanza Mama, tumempenda tunaomba aitwe Mama wa Taifa” “Mama, Taifa haliwezi kukamilika likiwa na Baba wa Taifa bila Mama wa Taifa, Watoto watakuwa na Malaria, na hapa hakuna ubaguzi, Rais wa kwanza Mwanaume Baba wa Taifa, Rais wa kwanza Mwanamke Mama wa Taifa na Mama kwakuwa ulipoenda Kanda ya Ziwa ulipewa cheo cha Uchifu na Wasaidizi wako wakakushauri ukakubali na hili la Mama wa Taifa haujataka wewe tunaomba utukubalie Kanda ya Kati” “Uzuri ni kwamba Mama unaowasaidia na wanaokupenda wanakuita Mama, uzuri wa pili unaowasaidia halafu wakakutukana nao wanakuita Mama , wewe sikiliza hotuba zao wakianza na tusi wanasema Mama, kwakuwa unazo sifa zote, Mama wa wote upendo wa wote, Mama umeenea”
0 Comments