Na Mwandishi Wetu, Bukoba
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Ndg. Mary Chatanda amewapokea wanachama 114 kutoka vyama vya upinzani katika Kata ya Katoro wilayani Bukoba Mkoani Kagera ambao wameona juhudi kubwa ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuleta Maendeleo makubwa katika Taifa.
Mwenyekiti Chatanda amewapokea Wapinzani hao jana katika ya Katoro na kusema matunda ya Rais Samia ndio yamefanya Wapinzani ndani ya wilaya ya Bukoba kuhamia CCM hivyo akawaomba viongozi wangu kuwapa ushirikiano mzuri katika kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinaendelea kukua zaidi .
"Nimefurahi kupokea wanachama wapya katika wilaya hii ya Bukoba maana kurudi kwa wapinzani sisi CCM ndio chachu ya kuongeza wanachama wapya katika wilaya yenu muwape ushirikiano wa kutosha kwa Maendeleo ya Chama chetu", amesema.
0 Comments